Timu ya Ufuatiliaji wa Miradi ya maendeleo kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo mnamo tarehe 09.10.2025, imetembelea baadhi ya miradi ya maendeleo yenye thamani ya zaidi Tsh. Milioni 938.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na
1. Ukamilishaji wa Kituo cha Afya Kata ya Ukondamoyo,
2. Ukamilishaji wa mabweni katika Shule ya Sekondari Kata ya Ukondamoyo
3. Ujenzi wa Njia za kutembelea (Walkways) katika kituo cha Afya Kata ya Vumilia,
4. Ujenzi wa Madarasa matatu Shule ya Msingi Mnadani Kata ya Mchikichini
5. Ujenzi wa vyumba 4 vya madarasa na matundu 9 ya Vyoo katika shule ya Msingi mnadani kata ya Mchikichini
6. Ukamilishaji wa Shule mpya ya Sekondari Muungano
Aidha katika ukaguzi wa miradi hiyo, timu hiyo ya ukaguzi wa miradi kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji ilisisitiza ufanisi na kasi katika ukamilishaji na ujenzi wa miradi hiyo, ili iweze kunufaisha wananchi wa Wilaya ya Urambo.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.