Urambo, Tabora
Watendaji wa Kata na Vijiji wa Wilaya ya Urambo, wamepongezwa kwa utendaji kazi wao mzuri na kuhakikisha Shughuli mbalimbali za Serikali zinatekelezwa kwa ufanisi hali inayoinua pato la Halmashauri ya Wilaya ya Urambo.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Bi. Grace Quintine, wakati akifunga kikao kazi cha Ukusanyaji wa Kodi ya majengo (Property TAX), ambapo kwa Mwaka wa fedha 2025/2026 Halmashauri ya Wilaya ya Urambo imeweza kukagua na kuthibitisha idadi ya Majengo 3120.
Aidha katika kikao hicho Bi. Grace Quintine amewapongeza Watendaji Kata na Vijiji wote kwa juhudi kubwa walizozionesha hadi kuweza kufikia idadi ya majengo 3120.
Sambamba na hilo, Bi. Grace Quintine ameendelea kuwapongeza kwa juhudi kubwa wanazozionesha katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Serikali ikiwemo Miradi ya maendeleo pamoja na ukusanyaji wa mapato, hali iliyopelekea pato la Halmashauri kuongezeka.
Aidha, Watendaji hao waliaswa na Mkurugenzi Mtendaji kuendelea kujiimarisha kiuchumi kupitia shughuli mbalimbali pamoja na fursa zilizopo Wilayani hapa, ili kujikwamua kiuchumi na kuweka kesho iliyo bora kwao.
Bi. Grace Quintine aliwaeleza kuwa Mtumishi wa Umma ni mfano katika jamii inayomzunguka, hivyo anapaswa kuishi maisha ya mfano na kujituma ili kuwa na pato lililobora na kuitengeneza kesho njema kwake.
Bomani Urambo
Anunani ya posta: Mkurugenzi Mtendaji (W), 30 Br ya Boma Stendi, S.L.P 170. 45582 Urambo Tabora
Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824
Simu ya mkononi: DED GRACE:0786821141
Barua pepe: ded@urambodc.go.tz
Copyright ©2025 Urambo . All rights reserved.