• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Urambo  District  Council
Urambo  District  Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Urambo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Maji
      • Elimu msingi
      • Elimu sekondari
      • Idara ya Mazingira
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Ufugaji Nyuki
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
    • Kata
      • Kata Zetu
    • Kibali cha Safari
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Watalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kiutumishi
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kamati ya Afya, Elimu na Maji
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya UKIMWI
      • Kamati Nyinginezo
        • Kamati ya Ugawaji wa Viwanja
        • Kamati ya Ajira
        • Kamati ya ALAT Mkoa
        • Wajumbe wa Mamlaka ya Mji Mdogo
    • Ratiba ya Vikao
    • Taarifa mbalimbali
  • Miradi
    • Miradi Mipya Itayotekelezwa
    • Miradi inayaoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Sheria
    • Taarifa
    • Taratibu
    • Zabuni
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Matukio
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video

DAS Urambo Awatoa Hofu Wananchi Juu ya NIDA

Siku iliyowekwa: April 30th, 2019

Katibu Tawala wa Wilaya ya Urambo Ndg Paschael Byemelwa amewatoa hofu wananchi wa wilaya ya Urambo juu ya upatokanaji wa vitambulisho vya Taifa-NIDA wakati akihutubia Baraza la wahe. Madiwani la uwasilishaji wa taarifa za kata tarehe 29.04.2019, katika ukumbi wa Halamashauri wilayani Urambo.

Akitoa ufafanuzi juu ya zoezi linaloendelea la ugawaji na uandikishaji wa wananchi wilayani Urambo, Ndg Byemelwa aliwaeleza wahe. Madiwani kutambua ya kuwa kila mkazi mwenyesifa  aliejiandikisha atapata kitambulisho cha Taifa-NIDA kwani zoezi la ugawaji na usambaji wa vitambusho hivyo linaendelea kwa kusimamiwa na maafisa wa NIDA walioko apa wilayani Urambo.

Ndg Byemelwa amewasihi wahe. Madiwani na watendaji wa kata kila mmoja kwa nafasi yake  kuwatoa hofu wananchi katika ngazi za vitongoji, vijiji na kata hasa kipindi hiki tunapoelekea katika usajili wa laini za simu za mawasiliano kwa kutumia alama za vidole yakuwa na imani na ofisi za NIDA kwani vitambulisho vinaendelea kutolewa pamoja na kuwepo kwa changamoto za hapa na pale.

Ndg Byemelewa alisema "zoezi hili la uandikishaji na utoaji wa vitambulisho linahitaji umakini sana ili kuhakikisha kitambulisho kinatolewa kwa raia wa Tanzania tu kwani kitatumika kama Kitambulisho cha Uraia  au Taifa na matumizi mengine mbalimbali yenye tija na maslahi kwa Taifa, na kuhusu usajili wa laini za simu za mawasiliano tayari Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amelitolea ufafanuzi hivyo halihitaji tena mjadala mrefu" alilisitiza Ndg Byemelwa. 

Aidha, Ndg Byemelwa amepongeza ushirikiano baina ya Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji na  Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Urambo wakati wa ugawaji wa jumla  ya vitambulisho 8125 vya wajasiliamali wadogo ilivyopokea kama mgao wa wilaya na tayari vitambulisho hivyo vyote vimetolewa kwa wajasiriamali wadogowadogo na kiasi cha Tsh 162,500,000/= (Milioni Miamoja Sitini na Mbili na Laki Tano) zilipatikana na zimepelekwa benki. Akitoa shukrani za pekee kwa Kitengo cha Biashara na kwa watendaji wa Kata na Vijiji, Ndg Byemelwa alieleza kuwa zoezi la ugawaji wa vitambuisho limefanikiwa kwa asilimia 100 kwani hakuna kitambulisho ata kimojo kilichopotea wala kiasi cha fedha ambacho hakikupelekwa benki.

Alkadhalika Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Urambo Ndg Adamu Malunkwi alimpongeza Katibu Tawala(W)  Urambo kwa ufafanuzi mzuri na wa kina wa upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa-NIDA kwa kuwa amewaondolea wahe. Madiwani sintofahamu iliyokuwepo na kuhaidi watawajulisha wananchi ili wawe na subira katika hilo. Pia Mhe. Malunkwi akionyesha uso wenye furaha na bashasha alipongeza mafanikio, ushirikiano na mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Ofisi ya  Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji(W)-Urambo kwani yamechangia kasi ya  ukamilishaji wa zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya wajasiliamali kwa  wakati; alisema vitambulisho hivyo  vitawasidiwa wajasiliamali wa Urambo kufanya biashara zao kwa amani, utulivu na  kuondokana na kero za kudaiwa ushuru kama ilivyokuwa awali.

 

Matangazo

  • Maotokeo ya Mtihani wa Kidato cha IV, II na Darasa la nne, 2020 January 15, 2021
  • Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato Cha I, 2021 December 18, 2020
  • Kuitwa Kazini Kada ya Afya July 09, 2018
  • Matokea Kidato cha Sita na Uwalimu July 13, 2018
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Sekondari 14 Urambo Zapata Huduma ya Intaneti

    October 20, 2019
  • Naibu Waziri Mgalu Apiga Goti Kuwashukuru Wananchi Urambo

    July 18, 2019
  • Pro.Ndalichako Akata Utepe VETA-Urambo

    July 09, 2019
  • Yaliyojili Urambo siku ya Meimosi

    May 01, 2019
  • Angalia zote

Video

Waziri wa maji, Prof. Makame Mbarawa
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Tovuti ya ofisi ya mkuu wa mkoa
  • FFARS USER GUIDE
  • PlanRep DOCUMENTATION
  • Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS)
  • Kata Zetu
  • BEMIS
  • Wahe. Madiwani

Tovuti mashuhuri

  • Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa
  • Tovuti ya sekretarieti ya Ajira
  • Fomu ya Maadili ya Viongozi kwa Mtandao
  • Public Service
  • Matokeo ya Mtihani wa Taifa Tanzania.
  • Ikulu

Waliotembelea Tovuti

world map hits counter

Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana nasi

    Bomani Urambo

    Anunani ya posta: S.L.P 170

    Simu ya mezani: +255 (0) 262 965 824

    Simu ya mkononi: 0784828287

    Barua pepe: ded@urambodc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2021 Urambo . All rights reserved.